>

TAIFA STARS KAMILI KWA AFCON

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ipo tayari kwa ajili ya AFCON 2023 inayotarajiwa kufanyika Ivory Coast ambapo tayari imeshawasili kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ameweka wazi kuwa kila mchezaji yupo tayari na wanaamini watafanya vizuri kwenye mechi ambazo watacheza.

Stars ilifanya mazoezi Stade Auguste Denis Est, San Pedro ikiwa ni kwa ajili ya kujiandaa na AFCON 2023, Ivory Coast.

Kocha huyo amesema:”Wachezaji wapo tayari na tunaamini kwamba yatakuwa na mashindano yenye ushindani mkubwa hivyo tupo tayari kwa ushindani,”.

N Januari 17 timu ya taifa ya Tanzania itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Morocco.

Januari 13 michuano mikubwa barani Afrika ya AFCON inatarajiwa kuanza kutimua vumbi, Ivory Coast.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini ni pamoja na Mbwana Samatta, Mzamiru Yassin, Dickson Job.