NI MUDA WA KUSHIRIKI NA SIO KUSINDIKIZA

TAYARI wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wamewasili nchini Ivory Coast kwa ajili ya kushiriki AFCON 2023, hii ni kubwa sana na inapaswa kuchukuliwa kwa ukubwa.

Hapa unaona kwamba kabla ya kuibukia Ivory Coast walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Misri na ilikuwa mechi nzuri licha ya Stars kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Kupoteza mchezo wa kirafiki haina maana kwamba kazi imekwisha hapana kuna kazi kubwa ambayo inafuata hapo ni muhimu wachezaji kufanyia kazi makosa yaliyopita kuwa imara zaidi.

Matokeo yanatafutwa ndani ya dakika 90 na sio kazi kubwa kushuhudia yule ambaye atapata maumivu ama kicheko mwisho hivyo kila mmoja atakuwa kwenye kibarua chake kupambania kombe.

Muda ni sasa kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya. Inawezekana kutokana na uwezo wa wachezaji ambao wameitwa kwenye timu ya taifa. Muhimu kushiriki kwa kuleta ushindani na sio kuwa wasindikizaji.

Ukweli ni kwamba kila mchezaji ana nguvu kubwa kwenye kusaka matokeo na ushindi kupatikana. Ambacho kinatakiwa kwa sasa ni kuwa makini kufuata maelekezo ambayo yanatolewa.

Wachezaji muda mfupi uliopo kwa ajili ya maandalizi utumike kwa umakini ili kuongeza furaha kwa Watanzania. Kushiriki AFCON na kupata matokeo mazuri ni jambo kubwa ambalo linapaswa kuandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu.

Waliopewa jukumu hilo ni wachezaji waliopo kambini na mashabiki kuendelea kuwaombea wachezaji wafanye vizuri kwenye kila mechi ambazo watashuka uwanjani.

Hakuna kukata tamaa kwa matokeo yaliyopita ama ugumu wa kundi ni kazi moja kutafuta ushindi mwanzo mwisho kwenye mechi hizi ambazo zitakuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Ipo wazi kuwa furaha ya mashabiki ipo kwenye matokeo mazuri na furaha ya wachezaji inabebwa na kupata ushindi ndani ya uwanja kwenye mchezo husika.

Muda wenyewe ni sasa na wachezaji wanatambua kwamba inawezekana kwa kuwa kupitia mazoezi ambayo wanafanya wanakuwa imara kwa ushindani kitaifa na kimataifa.

Nidhamu kubwa inahitajika wakati wa maandalizi hii itaongeza uelewa kwa wachezaji. Kufanya vizuri kwenye mazoezi kutaleta mwendelezo mzuri mpaka eneo la mechi ambayo ni kumalizia kazi iliyoanza kutengenezwa mwanzo uwanja wa mazoezi.

Majukumu ni mengi kwa kila idara na makosa yakiwa mengi ni rahisi kupoteza hivyo ni muhimu kupunguza makosa kwenye mechi ambazo zitachezwa uwanjani katika kusaka ushindi.

Inawezekana kupata ushindi kwenye mechi zote ikiwa wachezaji watajituma bila kuogopa na kupunguza makosa ndani ya uwanja huku wakitumia makosa ya wapinzani kupata ushindi.

Inafahamika kwamba mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa hivyo ni muhimu kwa wachezaji kupunguza makosa kila wakati na kuwa makini kutumia makosa ya wapinzani.

Yule ambaye atashindwa kutumia makosa ya mpinzani kwenye mchezo husika itakuwa rahisi kwenye kupoteza mchezo husika na kazi ipo kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake uwanjani.

Maandalizi mazuri yatakuwa silaha bora kupata ushindi kwenye mechi hizo zijazo ambazo zote zitakuwa ngumu kwani hakuna timu ambayo haipendi kupata ushindi uwanjani.

Benchi la ufundi pamoja na wachezaji ni muda wa kuongea lugha moja ya ushindi kuelekea kwenye mechi hizi ngumu kila mmoja anapaswa kutambua kwamba hakuna kinachoshindikana.

Wale ambao wanahofu hawapaswi kuwa nayo bali waamini kwamba kazi inakwenda kufanyika. Wachezaji walioitwa kwenye timu ya taifa wana uwezo na wanatambua kwamba taifa linawategemea.

Imani ni kuwa na uhakika kwa yale yajayo hata yakiwa magumu kwa namna gani hivyo ni muda wa kufanya kweli kupata ushindi kwenye mashindano haya makubwa.

Karibuni Temeke