NYOTA wa Mlandege FC kwake ni kicheko baada ya dakika 90 Januari 9 2024 kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya APR alipokomba milioni moja.
Wakati akiwa kwenye furaha ya kukomba mkwanja huo anasubiri mshindi kwenye mchezo wa nusu fainali kati ya Simba ama Singida fountain Gate hatua ya nusu fainali unaotarajiwa kuchezwa Januari 10.
Mkwanja huo alipokea kutoka kwa wadhamini Bima ya NIC ambao walipandisha dau la zawadi kutoka 750,000 hatua ya robo fainali.
Ni nahodha Abdallah Said alisepa na shilingi 1,000,000 kutokana na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Ipo wazi kwamba dakika 90 bao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Mlandege 0-0 APR na kwenye mapigo ya penalti ilikuwa Mlandege 4-2 APR FC.
Mlandege watakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye fainali Januari 13 wakisubiri mshindi wa mchezo wa leo Januari 10 kati ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate.