MSHAMBULIAJI wa Simba Jean Baleke kwenye kutimiza majukumu yake Mapinduzi 2024 alifunga bao pekee dakika ya 45+3 ambalo limekuwa ni ngazi kwa Simba kutiga hatua ya nusu fainali Mapinduzi 2024.
Januari 10 2024 inakwenda kupigwa nusu fainali ya kibabe kwa miamba hawa wawili ambapo Singida Fountain Gate wameweka wazi kuwa hawapo kinyonge tena.
Ikumbukwe kwamba mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Jamhuri walikuwa na mbinu ya kujilinda kwenye mchezo huo dakika zote 90 wakiwa nyuma ya mpira huku wakicheza kwa nidhamu kubwa.
Ipo wazi kwamba 2023 Simba iligotea katika hatua ya makundi hivyo imevunja rekodi yao ya mwaka uliopita.
Januari 10 itakuwa nusu fainali dhidi ya Singida Fountain Gate ambapo walipokutana katika hatua ya makundi ubao ulisoma Simba 2-0 Singida Fountain Gate.