OKRA KAMILI GADO, KUANZIA HAPA

BAADA ya kupata maumivu kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Yanga, hali yake kwa sasa inaendelea vizuri kwa Augustine Okra akitarajiwa kuwa kwenye kikosi cha nusu fainali  ama fainali kama watafika lakini atakosekana leo Januari 7.

Okra ambaye ni ingizo jipya alipata maumivu kwenye mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya KVZ ambapo alikwama kuendelea kwenye mchezo huo.

Leo Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa robo fainali dhidi ya APR kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainalli ambapo kocha msaidizi Mussa Ndaw ndani ya kikosi cha Yanga amesema kila kitu kipo sawa.

“Tunaamini utakuwa ni mchezo mgumu kwetu lakini tupo tayari na wachezaji wanatambua kazi kubwa iliyopo mbele ya wapinzani wetu tupo tayari.

“Alikuwepo hospitali kwa siku mbili, sasa amerejea hotelini…mashabiki watamuona In Shaa Allah nusu fainali au fainali”