UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa watawashtua wengi kwa mashine za maana watakazoshusha kupitia usajili wao wa dirisha dogo ambao umelenga kuboresha kikosi hicho kwenye mechi za ushindani.
Ipo wazi kwamba 2023 Simba ilifunga kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma KMC 2-2 Simba na mabao yalifungwa na Saido Ntibanzokiza na Jean Baleke ambaye kafikisha mabao 8 kwenye ligi, yale ya KMC yalifungwa na Wazir Junior.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameliambia Spoti Xtra kuwa mpaka Januari 15 watakuwa wamshatambulisha wachezaji wapya ambao watakuwa kwenye kikosi hicho kuongeza nguvu.
“Kwenye usajili wetu wa dirisha dogo nina uhakika tutawashtua wengi kutokana na aina ya wachezaji ambao tutawatambulisha, hawa wanakuja kufanya kazi kweli ukizingatia kwamba dirisha dogo halihitaji kusajili wachezaji wengi.
“Maboresho ambayo yanafanyika kwenye dirisha dogo ni maalumu kuongeza nguvu maeneo ambayo hayakuwa imara kidogo kutokana na sababu mbalimbali lakini tutawambulisha wachezaji wapya kabla ya Januari 15 mashabiki watawatambua,” alisema Ally.
Tayari Simba imetoa zawadi ya mwaka mpya 2024 kwa mashabiki wake baada ya kumtambulisha nyota mpya, Salehe Karabaka ambaye anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba kupitia dirisha hili dogo.