ENG HERSI SAID AKUTANA NA RAIS WA KLABU YA PARIS SAINT-GERMAIN YA UFARANSA

Rais wa Klabu ya Young Africans SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Januari 3, 2024.

Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.

Vilevile, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Eng Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0