>

OKRA KUANZA KAZI RASMI YANGA

BAADA ya kukamilisha usajili wa winga Mghana, Augustine Okra leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza kucheza kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi 2024.

Okra alizua gumzo kwenye mchezo wa funga mwaka 2023 kwa Yanga dhidi ya Jamhuri ambapo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Jamhuri 0-5 Yanga.

Leo Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa pili itakuwa dhidi ya Jamus FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku benchi la ufundi likibainisha kuwa litamtumia nyota huyo.

Kocha msaidizi wa Yanga, Mussa Ndaw ametoa uhakika kuhusu Augustine Okrah kutumika kwenye michuano hii ya Kombe la Mapinduzi 2024.

Kocha msaidizi wa Yanga, Mussa Ndaw alisema kuwa maandalizi yapo vizuri na winga mpya Agustino Okra yupo fiti na wataanza kumtumia kwenye Kombe la Mapinduzi 2024.

“Okrah yuko fiti na tuna mpango wa kumtumia kwenye mechi zijazo za michuano hii ukiwemo mchezo dhidi ya Jamus FC tunaamini utakuwa na ushindani mkubwa lakini tupo tayari,” alisema.