MABEKI wa Simba chini ya kiongozi wao Henock Inonga, Che Malone , Kenedy Juma wameingia kwenye mtengo kwa kuambiwa kwamba wanapaswa kutimiza majukumu yao na kuzuia kufungwa mabao.
Timu hiyo kwenye mchezo wa mwisho kwa 2023 dhidi ya KMC ilikwama kukomba pointi tatu na kugawana mojamoja dhidi ya KMC kutokana na kufungwa bao la jioni na mshambuliaji Wazir Junior aliyeweka usawa dakika ya 88.
Ipo wazi kuwa KMC walianza kufunga bao dakika ya 30 kupitia kwa Wazir Junior liliweka usawa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 56 kwa mkwaju wa penalti na Jean Baleke alifunga bao la pili dakika ya 57 ambalo wachezaji wa Simba walikwama kushikilia bomba.
Abdelhak Benchikha, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa ni muhimu kwa safu ya ulinzi kuongeza umakini kwenye kutimiza majukumu yao kwa kuzuia kufungwa mabao kwenye mechi wanazocheza.
“Ushindi ni jambo ambalo tunalihitaji kwenye mechi zetu na kupatikana kwa ushindi ni muhimu ulinzi na safu ya ushambuliaji kuwa makini.
“Ikiwa tutafunga kisha tukaruhusu sisi kufungwa hiyo itatufanya tusifikie malengo ambayo tunahitaji. Tuna muda wa kufanyia kazi hayo hivyo tunaamini kwa mechi zetu zijazo tutakuwa imara na kufanyia kazi makosa yaliyopita,” .