BENKI ya NMB imetoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya zawadi za mashindano ya kombe la mapinduzi Zanzibar na Traki suti 150 kwa ajili ya kuvaa kwenye matembezi siku ya Mapinduzi.
Fedha hizo kwa ajili ya bingwa ambaye atazoa shilingi milioni 100 mshindi wa pili milioni 70, pamoja na medali za mabingwa na mshindi wa pili.
Akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi nguo za mazoezi kwa ajili ya siku ya mazoezi kitaifa yatakayofanyika Januari 1, ambazo zilimetolewa na benki hiyo Meneja Biashara Zanzibar benki ya NMB Naima Said Shaame .
Alisema udhamini huo unalenga azma ya benki ya NMB na pia juhudi za Serikali katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema benki ni miongoni wa wadau wakubwa inayochangia ukuaji wa wa sekta mbalimbali za maendeleo Zanzibar, hivyo waliona ni wajibu wao kuwa sehemu ya maadhimisho ambayo kilele chake ni Januari 12.
‘’Kama Benki tunasema huu sio mwisho wa udhamini wetu. Tunaamini kwamba michezo sio tu inachangia ustawi wetu, lakini pia inatuleta pamoja kama taifa’’aliongeza.
Amesema NMB imeamua kutoa Traki suti hizo za mazoezi 150 kwa jili ya kuunga mkono siku ya mazoezi ikitaifa jambo ambalo hulifanya kila mwaka, kuonyesha kuwa mazoezi ni muhimu kwa wananchi ambao ni wateja wao.
‘’Tunapenda kuwa na wateja wenye afya na tunajua kuwa mazoezi ni afya, hivyo tumeamua kuunga mkono jambo hilo ili kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na afya njema,” amesema
Akizungumza baada ya kupokea Traki suti hizo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab, aliishukuru benki ya NMB kwa misaada mbali mbali inayotoa.
Amesema benki hiyo ni kiongozi wa kutoa misaada kwa serikali katika nyanja zote za michezo na jamii, hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka kwani siku ya mzoezi ya kitafa ni siku kubwa.
Katibu Fatma alisema amepokea misaada hiyo kwa furaha, ambapo ameitaka benki hiyo kuendelea kusaidia kwani bado kuna mahitaji mengi yanatakiwa kuendeleza michezo Zanzibar.