>

YANGA YAPIGA HESABU NDEFU BONGO

HESABU ndefu za Yanga ndan kutwaa ubingwa ambao upo mikononi mwao waliotwaa msimu wa 2022/23.

Chini ya Miguel Gamondi Yanga ilitoka kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kinara wa utupiaji wa mabao ni Aziz KI ndani ya Yanga na ligi kiujumla akiwa katupia mabao 9 kibindoni ambapo kwenye mabao hayo alifunga hat trick moja kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa kikubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zote wanazocheza ili kupata matokeo chanya.

“Kikubwa kwenye mechi za ligi tunahitaji matokeo mazuri ambayo yatatufanya tufikie malengo yetu ya kutwaa ubingwa inawezekana kutokana na wachezaji waliopo.

“Benchi la ufundi furaha yao ni kuona matokeo yanapatikana hivyo tu basi. Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zote ambazo tunacheza,” alisema Kamwe.

Baada ya kucheza mechi 10 Yanga kibindoni ina jumla ya pointi 27 vinara wakiwa ni Azam FC wenye pointi 31 baada ya kucheza mechi 13.