>

SIMBA NA KMC ZAPIGANA MKWARA WA POINTI TATU

WAKIWA kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara Desemba 23 Uwanja wa Azam Complex wababe kutoka Dar wamepigana mikwara.

Ni KMC watawakaribisha Simba kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Abdihamid Moallin Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa wanatambua ugumu uliopo lakini wanapaswa kuamini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Tunatambua utakuwa mchezo mgumu na ushindani lakini tunapaswa kuamini kwamba tutapata ushindi kwenye mchezo huo kwa kuwa maandalizi yapo sawa,”.

Kwa upande wa Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu.

“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya KMC na tunahitaji kupata pointi tatu muhimu,”.