>

KOCHA KAGERA SUGAR AKUTANA NA MKONO WA ASANTE

UONGOZI wa Kagera Sugar umeweka wazi kuwa umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Mecky Maxime aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Maxime mchezo wake uliopita ilikuwa ni Desemba 21 ambapo alishuhudia ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 0-4 Azam FC.

Unakuwa ni mchezo wa tatu kupoteza baada ya kuanza kushuhudia Coastal Union 1-0 Kagera Sugar, Simba 3-0 Kagera Sugar na Kagera Sugar 0-4 Azam FC.

Taarifa imeeleza kuwa kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya kocha msaidizi Marwa Chamberi.