>

AZAM FC YAZIDI KUPETA BONGO

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamezidi kupeta kwenye mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na kuendeleza kasi ya ushindi kwenye mechi ambazo wanachea.

Desemba 21 ikiwa ugenini iliibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao Kagera Sugar.

Pointi tatu walizopata Azam FC dhidi ya Kagera Sugar zinawazidi kuwafanya wajikite nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya dakika 90 ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-4 Azam FC. Ni Feisal Salum alianza kufunga dakika ya 9, Prince Dube dakika ya 11, Pascal Msindo dakika ya 45 na Allasane Diao dakika ya 84.

Pointi 31 ni mali ya Azam FC baada ya kucheza mechi 13 ikifuatiwa na Yanga nafasi ya pili pointi 27 baada ya kucheza mechi 10 huku Simba nafasi ya tatu na pointi 22 baada ya kucheza mechi 9.