ZILIZOPO MKIANI MUHIMU KUONGEZA JUHUDI

KAZI ni kubwa kwenye mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na kila timu kuonyesha uwezo wake kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

Ipo wazi kuwa mzunguko wa kwanza kila timu inapambania malengo yake huku baadhi ya timu zikiwa kwenye nafasi ya mwisho wengi hupenda kuita nafasi ya mkiani.

Kikubwa ambacho kinatakiwa kwa timu zote ambazo zipo kwenye nafasi hizo ni kupambana kujinasua kutoka hapo ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo.

Ukweli ni kwamba hakuna ambaye anapenda kuona wanashindwa kupata matokeo chanya lakini ni muhimu kufanya kweli bila kuchoka.

Muda ni sasa kwenye kutimiza majukumu ili kupata pointi tatu. Inawezekana kwa kila timu kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri.

Ili kuepuka janga la kushuka daraja itakuwa ngumu kwa timu hizo kupata nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara muda uliopo ni kukamilisha mpango kazi kwa kupata pointi tatu.

Vita ni kubwa kwa kila timu kujitahidi kutimiza majukumu yake hivyo kinachotakiwa ni kuwa makini kwenye nafasi ambazo zinapatikana na kufanyia kazi makosa yaliyopo kwenye timu husika.

Kufanyia kazi makosa hayo itakuwa ni hesabu kubwa kupata ushindi kwa mechi zijazo kutokana na kila mmoja kuwa tayari kufanya vizuri ndani ya uwanja.

Kilala kheri timu zote ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Championship kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.