>

ZAMU YA YANGA KUWAPA FURAHA MASHABIKI

KIMATAIFA mwendo ni mbovu kwa timu zote mbili ambazo zimetinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na picha ya mechi za tatu za awali ilivyokuwa.

Katika safu ya ushambuliaji inaonekana matatizo ni makubwa kwa timu zote na hata ulinzi pia ni shida hivyo ni muhimu benchi la ufundi kufanyia kazi.

Yanga na Simba hawa ni wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa kila mmoja akipambana kufikia malengo yake ya kutinga hatua ya robo fainali.

Sio kazi nyepesi kutokana na ushindani uliopo na ili kupata matokeo ni lazima kushinda ndani ya dakika 90.Leo ni zamu ya Yanga kuwapa furaha mashabiki wa Tanzania.

Afrika Mashariki inasubiri kuona furaha kutoka kwa Yanga kwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeana na inawezekana ikiwa wachezaji wataamua kujituma na kupunguza makosa.

Kikubwa ni kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kupunguza makosa ndani ya uwanja ili kuwa na nafasi ya kupata matokeo ikiwa nafasi ambazo zitapatikana zitatumika.

Muda uliopo ni sasa na kila mchezaji atambue kwamba furaha ya mashabiki inabebwa na matokeo mazuri. Hakuna mchezaji anayependa kuona timu inapoteza ipo hivyo hata kwa mashabiki pia.

Iwe kheri kwa Yanga na benchi la ufundi kwa wachezaji kujituma bila kuogopa kutafuta matokeo ndani ya uwanja, muda ni sasa.

Tumeona namna Simba walivyozinduka na kucheza kwa ushirikiano dhidi ya Wydad Uwanja wa Mkapa licha ya kupata ushindi bado haijaisha mpaka iishe..