YANGA YAGOMEA JAMBO HILI CAF

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa haujakata tamaa kwenye mashindano ya kimataifa malengo yao bado yapo kuona kwamba wanafikia hatua ya robo fainali.

Katika mechi tatu ambazo ilicheza, Yanga ilivuna pointi mbili na safu ya ushambuliaji ilitupia mabao mawili huku ile ya ulinzi ikiruhusu mabao matano.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa malengo makubwa ni kupata matokeo kwenye mechi zilizobaki ili kutinga hatua ya robo fainali.

“Bado tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zetu za nyumbani kwa kuhakikisha kwamba tunapata pointi tatu muhimu. Hakuna kukata tamaa kwa kuwa mipango inaendelea na nafasi bado ipo.

“Mashabiki wanapaswa kuelewa kwamba kila hatua ushindani ni mkubwa na wao jukumu lao ni kuwa na mwendelezo uleule wa kuwa bega kwa bega na timu tunaamini tutafanikiwa malengo yetu,”.

Mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Yanga ni dhidi ya Medeama unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Desemba 20.