YANGA 3-0 MEDEAMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

BAADA ya dakika 90 kuukamilika, Yanga imeshinda mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Medeama wakiwa nyumbani.

Ni mabao 3-0 Yanga wameshinda baada ya Pacome kufungua ukurasa wa mabao kipindi cha kwanza na Bakari Mwamnyeto na Mudathir Yahya kufunga kwenye mchezo wa leo kipindi cha pili.

Kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa Yanga walianza  kwa kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Medeama ya Ghana.

Ni bao la nyota Pacome Zouzoua ambaye kafunga katika kipindi cha kwanza muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.

Ilikuwa dakika ya 33 nyota huyo wa kazi alipachika bao hilo lililowanyanyua mashabiki wa Yanga.

Bao hilo linawapa uongozi Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi katika msako wa kutinga hatua ya robo fainali Afrika.

Kiungo wa kazi Mudhathir Yahya ameanza katika kikosi cha kwanza huku mwamba Kennedy Musonda, Yao, Dijigui Diarra nao wakiwa katika kikosi.

Katika eneo la ukabaji ni kiungo Khalid Aucho anatimiza majukumu yake Uwanja wa Mkapa.