NAMNA SIMBA WALIYVOANZA KUONANA KIMATAIFA/ BADO MMENUNA

KWENYE anga la kimataifa Simba wamepata ushindi wa kwanza msimu wa 2023/24 dhidi ya Wydad Casablanca kwa mabao ya kiungo mshambuliaji Willy Onana ambaye alipachika mabao yote mawili. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Onana alitumia pasi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Kibu Dennis.

Simba inafikisha pointi tano ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo ikitoka kuonja ladha ya kuwa mkiani baada ya kufungwa dhidi ya Wydad mchezo wake uliopita.