TABORA UNITED YAPELEKA ONYO JANGWANI

UONGOZI wa Tabora United zamani ikijulikana kama Kitayose umesema kuwa kampeni ya kuzisaka alama tatu dhidi ya Yanga imeanza, huku wakiamini kuwa kuanza maandalizi mapema ndiyo njia pekee yakutimiza malengo waliyojiwekea katika mchezo huo.

Pendo Lema ambaye ni Afisa habari wa klabu ya Tabora United amesema kuwa kwa sasa hawana muda wakupoteza, na tayari kikosi kimeanza mazoezi mapema kuwinda alama tatu muhimu dhidi ya Yanga.

Tumeanza mazoezi mapema jana kikosi chetu chote kipo kambini tayari mazoezi yamepamba moto, wachezaji wanamorali kubwa mazoezini kuonyesha kuwa wana nia kubwa kutwaa pointi tatu dhidi ya Yanga

Tunajua kuwa itakuwa mechi ngumu kutokana na ubora wa timu ya Yanga kwa sasa, tumeanza mazoezi mapema maana hatuna chakupoteza safari hii Yanga wanakuja Katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kucheza mechi ya kihistoria na timu pendwa ya wananchi wa Tabora.

Mwalimu Gorani amesema Hana shaka na wachezaji kutokana na kiwango wanachoonyesha mazoezini na katika mechi zilizopita”.alisema Pendo

Mchezo wa Tabora United na Yanga unatarajiwa kupigwa Disemba 22, 2023 katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora.