SIMBA YAWATULIZA WAARABU KWA MKAPA

MCHEZO wa nne kwa Simba katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanavuna pointi tatu ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Simba 2-0 Wydad Casablanca.

Katika mchezo wa leo Desemba 19 mabao yote ya Simba yalifungwa kipindi cha kwanza cha mchezo ndani ya dakika 45 na kuvuna pointi tatu wakiwa nyumbani.

Ni Willy Onana alipachika mabao yote dakika ya 36 na 37 akiwanyanyua mashabiki wa Simba licha ya kukwama kukomba dakika 90 baada ya kupata maumivu.

Ushindi huu ni wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdelhackh Benchikha ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa leo.

Simba sasa inafikisha pointi tano ikiwashusha Wydad Casablanca ambao wana pointi tatu wote wakiwa wamecheza mechi nne.

Matokeo ya mchezo kati ya ASEC Mimosas vinara wa kundi dhidi ya Jwaneng Galaxy yatatoa picha kamili ya uwezekano wa Simba kupata nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.