SIMBA NA YANGA KIMATAIFA NGUVU YA ZIADA INAHITAJIKA

NGUVU ya ziada inahitajika kwa Simba na Yanga kutusua kimataifa. Kwenye soka lolote linawezekana hivyo tusiwakatie tamaa. Kwenye mechi tatu ambazo ni dakika 270 timu zote mbili zimekomba pointi mbili jambo linaloongeza ugumu kwao kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali ikiwa watapoteza mechi zote.