SIMBA 2-0 WYDAD LIGI YA MABINGWA AFRIKA

DAKIKA 45 za mwanzo Simba wanakwenda kwenye vyumba vya mazungumzo wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0 Wydad Casablanca ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtupiaji wa mabao yote mawili ni kiungo mshambuliaji Willy Onana ambaye kafunga mabao hayo ndani ya dakika mbili.

Alianza dakika ya 36 na lile la pili ilikuwa dakika ya 38 akiwanyanyua mashabiki wa Simba waliojitokeza kushuhudia mchezo wenye ushindani mkubwa.

Viungo wawili Saido Ntibanzokiza na Sadio Kanoute wanaukosa mchezo wa leo kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano.