VIUNGO wawili wa kazi ndani ya kikosi cha Simba watakuwa mashuhuda Uwanja wa Mkapa Simba ikisaka matokeo kwenye mchezo dhidi ya Wydad ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi.
Ni Sadio Kanoute kiungo mgumu aliyepata kadi tatu kwenye mechi tatu mfululizo alianza mchezo dhidi ya ASEC Mimosas Uwanja wa Mkapa ngoma ikawa dhidi ya Jwaneng Galaxy ugenini na ile ya tatu dhidi ya Wydad.
Mbali na Kanoute kiungo mkali wa mapigo huru ndani ya Simba Saido Ntibanzokiza naye pia atakuwa jukwaani kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano.
Ntibanzokiza ni yeye aliyefunga bao kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas kwa mkwaju wa penalti likiwa ni bao pekee kwa Simba hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270.