MAXI Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga ameweka wazi kuwa yeye sio mtu wa manenomaneno mengi bali atafanya kazi kwa vitendo.
Kiungo huyo ndani ya Ligi Kuu Bara ni namba mbili kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga akiwa katupia mabao 7 kinara ni Aziz KI mwenye mabao 9 kibindoni.
Desemba 20 Yanga inatarajiwa kuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Nzengeli amesema:”Sipendi kuwa mtu wa ahadi ama manenomaneno mengi hapana, mashabiki wa Yanga waapenda burudani na wapo na timu kila wakati hivyo kazi yetu itakuwa ni kwa ushirikiano.
“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza tunaamini kwamba watapata furaha na sisi tutapambana kupata matokeo mazuri,”.