KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amefumua kikosi hicho ambapo wachezaji wawili watakuwa jukwaani ikiwa ni Sadio Kanoute na Saido Ntibanzokiza wanaoutumikia adhabu ya kati tatu za njano.
Mchezo wa leo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili ambazo zinasaka pointi tatu muhimu.