CHAMA ASABABISHA MAJANGA KWA WAARABU

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amesababisha majanga kwa Waarabu wa Morocco Wydad Casablanca kwa kuwa chanzo cha nyota wao kuukosa mchezo wa marudiano Dar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 19 saa 10:00 jioni.

Simba iliyo kundi B mwendo haijawa kwenye mwendo bora kutokana na kushindwa kupata ushindi katika mechi tatu za hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilizocheza.

Ni mechi mbili iliambulia sare ilianza Simba 1-1 ASEC Mimosas na Jwaneng Galaxy 0-0 Simba, ilipoteza mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi kwa kufungwa bao 1-0 Wydad Casablanca.

Chama aliingia kipindi cha pili akitokea benchi dakika ya  58 akichukua nafasi ya Willy Onana alichezewa faulo dakika ya 62 na nyota Yahya Jabrane ambaye alionyeshwa kadi ya njano.

Inakuwa ni kadi yake ya tatu ya njano kuonyeshwa nyota huyo kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo hatakuwa kwenye kikosi kitakachowavaa Simba Desemba 19 Uwanja wa Mkapa.