Skip to content
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zao ni kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.
Huo ni mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali wakiwa wamecheza mechi tatu na kukusanya pointi mbili kibindoni.
Desemba 20 Yanga wanatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa baada ya ule waliochez ugenini kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Ali Kamwe Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao na wanahitaji matokeo mazuri.
“Baada ya mchezo wetu wa jana wa ligi wachezaji wanarejea uwanjani leo kuanza maandalizi kuelekea mchezo wetu ujao dhidi ya Medeama.
“Mashabiki ni wakati wao kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo kwa kuwa tayari GSM kwenye mchezo huo amenunua viti vyote vya mzunguko.
“Mechi hii itakuwa ni ya tofauti zile zilizopita ilikuwa kawaida kuipa jina la mchezaji ya sasa itakuwa ni GSM Day,”.