NGUVU YA AZAM FC YAGEUZWA HUKU

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa baada ya kupata matokeo kwenye mechi zao za ligi sasa wanageukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Azam FC mchezo wake uliopita wa ligi ilishinda kwa mabao 2-1 JKT Tanzania inakibarua  na Alliance ya Mwanza, kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo. Mchezo huo unachezwa Uwanja wa Azam Complex, Jumapili hii Desemba 17, saa 11.00 jioni.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wanatambua ushindani ulivyo kwenye mashindano ya ASFC kwa kuwa ni mtoano watapambana kupata matokeo.

Tunahamishia nguvu kwenye ASFC mashindano ambayo ukipoteza mchezo mmoja hautakuwa na nafasi ya kuendelea hivyo tahadhari zote tunazichukua na tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi,”.

Kwenye mchezo huo ambao Azam FC na Alliance zote zinahitaji ushindi kwenye kikosi cha kwanza cha Azam FC ni Foba ameanza langoni, Chilambo, Daniel Amoha yeye ni nahodha, Manyama,Sidibe, Bangala, Sopu, Akamiko, Allasane, Lyanga na Nado wameanza kikosi cha kwanza.