>

SIMBA YAMALIZANA NA WINGA WA MABAO

INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba umemalizana na winga wa mabao ndani ya Mtibwa Sugar, Ladack Chasambi.

Nyota huyo jina lake lipo pia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambacho kilikuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mechi za kimataifa hivi karibuni.

Ilikuwa ni kwenye kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia ambapo kiungo huyo alijumuishwa katika kupeperusha bendera ya Tanzania.

Miongoni mwa timu ambazo kazifunga ndani ya Ligi Kuu Bara ni pamoja na Geita Gold.

Habari zinaeleza kuwa tayari nyota huyo mwenye pasi tatu za mabao ndani ya ligi amefikia makualiano mazuri na Simba.

Ikiwa dili lake litajibu huenda katika dirisha dogo akatambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kuanza majukumu yake mapya kwa msimu wa 2023/24 akiwa na uzi wa Simba.