IPO wazi kuwa mtambo wa kazi uliotambulishwa ndani ya Yanga ni noma kutokana na majukumu yake kuwarahisishia kazi benchi la ufundi la timu hiyo.
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameongezewa mtu mwingine wa kazi kwaajili ya kuongeza nguvu kwenye kusaka ushindi.
Ni Mpho Maruping kutoka Afrika Kusini ambaye Desemba 14 alitambulishwa rasmi kuwa ni Mtaalamu wa Kusoma Video za Wapinzani (Video Analyst) wa kikosi hicho.
Mpho amewahi kuwa mchezaji katika vilabu mbalimbali vya ligi kuu nchini humo na kabla ya kutimkia Yanga alikuwa akihudumu kama Mtaalamu wa Kusoma Video za wapinzani kwa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) iliyofanikiwa kuchukua Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON 2022) na ile iliyofika 16 Bora ya Kombe la Dunia kwa Wanawake 2023 nchini Australia.