KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Meck Mexime amesema kuwa anawatambua wapinzani wao Simba namna walivyo bora na wachezaji walivyo na akili katika kutimiza majukumu yao hivyo wataingia kwa tahadhari.
Maneno ya kocha huyo ni kama mtego kwa Simba kutokana na mpango kazi ambao wanao Kagera Sugar kusepa na pointi tatu mbele ya Simba na ikumbukwe kwamba mechi ya Simba na Kagera Sugar haijawahi kuwa rahisi.
Desemba 15 2023 Kagera Sugar iliyotoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani itavaana na Simba iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo mchezo wao wa ligi uliopita.
Maxime ameweka wazi kuwa mashabiki wanasema kuhusu timu hiyo ilivyo kwenye mwendo usio mzuri pamoja na ratiba kuwa ngumu kwao lakini wanatambua uimara wa Simba.
“Wametoka kucheza mechi kubwa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Waarabu wenyewe na wanapishana nao, hivyo ni aina ya mchezo mgumu tunawaheshimu Simba.
“Watu wa mpira tunajua hivyo hakuna ambaye anawabeza na wachezaji wetu wanatambua hilo kikubwa ni kusubiri na kuona namna itakavyokuwa uwanjani,”.