>

SINGIDA FOUNTAIN GATE SASA NI BLACK RHINO

UONGOZI wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa hasira zote walizoanza nazo kuoyesha Uwanja wa Liti kwa mechi zao za nyumbani zinahamia Uwanja wa Black Rhino.

Uwanja huo wa Black Rhino Academ upo Karatu utatumiwa na Singida Fountain Gate baada ya Uwanja wa Liti kufungiwa kutokana na kukosa ubora.

Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza amesema kuwa bado wanaendelea kusubiri taarifa zaidi kuhusu Uwanja wa Liti lakini wameshapata uwanja mbadala.

“Tutautumia Uwanja wa Black Rhino wa Karatu mpaka pale uwanja wa CCM Liti wa mjini Singida utakapokuwa tayari tena kwa matumizi ila kazi kubwa itafanyika kwenye mechi zetu zote kutafuta ushindi.

Tuna mechi mbili ambazo zipo karibu hizo tutatumia uwanja huo itakuwa ni Desemba 11 dhidi ya KMC na Desemba 15 dhidi ya Arusha FC mchezo wa Kombe la Azam Sports Federatio,”.

Taarifa ambayo imetolewa na Singida Fountain Gate Desemba 10 imeeleza kuwa mapato yote ya klabu katika mchezo dhidi KMC yatakuwa ni maalumu kuchangia kwenye kusaidia ndugu walioathirika na mafuriko, Hanang, Manyara.