MTIBWA SUGAR YAPOTEZA TENA UGENINI

HAIJAWA kwenye mwendo mzuri Klabu ya Mtibwa Sugar ndani ya msimu wa 2023/24 kutokana na kukwama kupata pointi tatu ugenini.

Desemba 7 ikiwa ugenini imepoteza pointi tatu dhidi ya Namungo FC kwa kushuhudia ubao ukisoma Namungo 1-0 Mtibwa Sugar.

Bao la ushindi lilifungwa Derick Mukombozi ambapo Mtibwa Sugar ilitoka kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam FC kwa kufungwa mabao 5-0.

Ni pointi tano imekusanya timu hiyo msimu wa 2023/24 ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.