WAMEKUTANA NA BALAA LA BENCHIKHA HUKO SIMBA, CHAMA, BALEKE

BENCHI la ufundi la Simba china ya Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha limeweka wazi kuwa ni muhimu kwa nyota wake ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Saido Ntibanzokiza kwenye safu ya kiungo Jean Baleke kwenye safu ya ushambuliaji kuongeza kasi kwenye eneo la wapinzani katika matumizi ya nafasi ambazo wanazipata.

Mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika Simba haijapata ushindi zaidi ya kuambulia sare kituo kinachofuata ni dhidi ya Wydad Casablanca mchezo unaotarajiwa kuchezwa Desemba 9 2023.