BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo imefuzu kucheza mashindano ya WAFCON 2024 yatakayofanyika nchini Morocco.amesema kuwa jitihada za kupata ushindi zilishindikana lakini wachezaji walijituma.
Twiga imefuzu baada ya ushindi wa jumla wa mabao 3-2 dhidi ya Togo ambapo kila mmoja kashinda kwenye mechi aliyokuwa nyumbani.
Ikumbukwe kwamba Twiga Stars kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-0 na Desemba 5 ilipoteza ugenini kwa mabao 2-0.
Ushindi wa jumla inakuwa ni Tog 2-3 Tanzania, hivyo kazi bado inaendelea kwa Twiga Stars kufanya vizuri hatua inayofuata.
Shime amesema:”Tulikuwa na nafasi kupata ushindi kipindi cha kwanza lakini nafasi ambazo tulizitengeneza wachezaji hawazikutumia, kipindi cha pili pia ilikuwa hivyo tukaamua kuongeza nguvu kwenye ulinzi.
“Ninawapongeza wachezaji kwa hili lililotokea makosa tutayafanyia kazi kwa ajili ya kuendelea kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata,”