BAADA ya Yanga na Simba kucheza mechi mbili katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ipo wazi kwamba wameanza kwa kusuasua hivyo ni muhimu wafanye kweli kwenye mechi nne zilizobaki.
Ikiwa watazichanga karata vyema katika mechi nne zilizobaki angalau wanaweza kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali ambayo ni kazi ngumu kutokana na makundi waliyopo pamoja na pointi walizonazo. Hizi ni mechi nne ambazo zitawabeba ikiwa watapata matokeo chanya kimataifa