>

SIMBA WAWAFUATA WAARABU MOROCCO

WAWAKILISHI  wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Simba Desemba 5 2023 imeenza safari yakuelekea Morocco.

Safari hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuikabili timu ya Wydad Casablanca mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita kwa Simba wakiwa ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy walishuhudia ubao ukisoma Jwaneng Galaxy 0-0 Simba.

Katika dakika 90 waligawana pointi mojamoja hivyo baada ya kucheza mechi mbili, Simba ina pointi mbili kibindoni kwenye hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Desemba 9, 2023 Simba watakuwa ugenini.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni kipa Ayoub Lakred, Kennedy Juma, Clatous Chama, Shomari Kapombe.