SIMBA KAZI IPO, KUWAVAA WAARABU WENYE NJAA

BAADA ya kuvuna pointi moja ugenini ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hesabu za wawakilishi wa Tanzania ni mchezo wao ujao dhidi ya Wydad Casablanca.

Kibarua kigumu kwa Simba kukutana na Waarabu wa Morocco wenye njaa ya kupata ushindi wakati Simba wakiwa kwenye mwendo wa kusuasua katika kupata matokeo.

Desemba 3 2023 kikosi cha Simba kiliwasili Dar kikitokea nchini Botswana kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy ambapo katika mchezo huo ubao ulisoma Jwaneng 0-0 Simba.

Baada ya mchezo huo Simba inaanza hesabu za kuchukua pointi tatu ugenini ikikutana na Wydad Casablanca Desemba 9, 2023 nchini Morocco.

Simba ina pointi mbili huku Wydad ikiwa mkiani bila pointi baada ya kufungwa mechi mbili katika kundi B.

Kazi ni nzito kwa Simba iliyo kwenye hesabu za kuwania kutinga robo fainali kutokana na kushindwa kupata ushindi kwenye mechi zake mbili mfululizo ikiambulia pointi mbili.