>

YANGA: BURUDANI INAREJEA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa burudani inarejea mahali pake baada ya kukosekana kwa muda ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Desemba 2 2023 Yanga inatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kumenyana na Waarabu wa Misri, Al Ahly ukiwa ni mchezo wa hatua ya makundi.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga amesema kuwa walianza kwa kupoteza ugenini lakini wanarejea kuendelea burudani.

Tulitoka kuelekea kwenye majukumu ya nchi ugenini tukapoteza pointi tatu lakini wachezaji walipambana, sasa tunarudi Uwanja wa Mkapa ikiwa ni burudani inarudi mahali pake.

Mashabiki ambao walikosa burudani kwa muda ni wakati wao kushuhudia namna ambavyo wachezaji watacheza kwa juhudi kutafuta ushindi kwa kuwa tutakuwa nyumbani.

Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yanahitaji umakini mkubwa iwe nyumbani ama ugenini. Sisi tupo tayari na tunaamini tutapata matokeo,” alisema Kamwe.

Novemba 24 kete ya kwanza kwa Yanga ilikuwa ugenini walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.