UONGOZI wa Tabora United umeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kupata pointi tatu dhidi ya wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Desmba Mosi ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili ndani ya mwezi mpya Desemba.
Ofisa Habari wa Tabora United, Pendo Lema amesema kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar wapo tayari kukabiliana na wapinzani hao ndani ya dakika 90 kusaka ushindi.
“Tunatambua mchezo wetu ujao utakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar maandalizi yapo vizuri kuhakikisha kwamba tunapata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu. Wachezaji wapo vizuri isipokuwa tutamkosa Kelvin Kingu Pemba aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida Fountain Gate.
“Wembe ni uleule kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar na tutakuwa nyumbani Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi sio salama kwa wapinzani wetu watatuachia pointi tatu muhimu ambazo tunazihitaji,” amesema Pendo.