>

RAIS YANGA MWENYEKITI WA CHAMA CHA VILABU AFRIKA

NI Rais wa Yanga SC, Hersi Said amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Vilabu barani Afrika (African Clubs Association – ACA), katika uchaguzi uliofanyika leo nchini Misri.

Hersi atasaidiwa na makamu wenyeviti wawili ambao ni Jessica Motaung wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Paul Bassey kutoka Akwa United ya Nigeria.

Kila la kheri Injinia kwenye majukumu mapya katika familia ya michezo.