LUIS BADO ANAENDELEA KUJITAFUTA

TAYARI ameanza kurejea katika hesabu za rekodi lakini maamuzi bado anajitafuta kufikia ubora wake wa 2021 aliposepa ndani ya kikosi hicho na kujiunga na Al Ahly ya Misri.

Kukaa muda mrefu bila kucheza ni sababu iliyofanya kiwango chake kikaporomoko kwa kasi.

Yule Luis Miquissone mwenye kasi ya haraka na maamuzi akiwa nje ama ndani ya 18 bado anajitafuta.

Simba ikiwa imetupia mabao 16 katika mechi sita katoa pasi tatu za mabao na mechi zote waoikomba pointi tatu.

Dhidi ya Mtibwa Sugar alimpa Clatous Chama ikiwa ni pasi yake ya kwanza, Singida Foutain Gate na Ihefu alitoa pasi mojamoja mtupiaji akiwa ni Moses Phiri.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba hivi karibuni aliweka wazi kuwa bado nyota huyo hajawa kwenye ule ubora wake asilimia kubwa.

“Taratibu anazidi kuimarika na akichanganya atafanya kazi kubwa uwanjani kwa kuwapa furaha mashabaiki,”.

Kituo kinachofuata ni Novemba 5 2023 Simba v Yanga.