KIUNGO wa kazi Yahya Zaid bado yupo sana ndani ya kikosi cha matajiri wa Dar Azam FC bado yupo sana kwenye kikosi hicho.
Nyota huyo ameongeza dili la miaka miwili kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho.
Mwamba ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026.
Kasi ya Azam FC kwa msimu wa 2023/24 taratibu imeanza kupungua baada ya kukwama kushinda kwenye mechi mbili mfululizo ugenini na nyumbani.
Ilipoteza dhidi ya Yanga kwenye Mzizima Dabi mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa wakati najitafuta lipoteza dhidi ya Namungo ikiwa nyumbani.
Bado ina nafasi ya kurejea kwenye makali yake kwa kuwa ligi bado ipo mwanzo ikiwa ni wiki ya saba na wiki ya nane Azam FC itakuwa ugenini dhidi ya Mashujaa ya Kigoma.