SIMBA YAMCHAPA MBABE WA MTANI

POINTI tatu Simba wamezikomba mbele ya mbabe wa mtani wao wa jadi, Yanga kwa msimu wa 2023/24  ambaye ni Ihefu.

Ni mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa Oktoba 28 2023 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-1 Ihefu.

Mabao ya Simba yalifungwa na Jean Baleke dakika ya 13 likawekwa usawa na Ismail Mgunda dakika ya 25 na kufanya kipindi cha kwanza wote watoshane nguvu.

Bao pekeee lililowapa Simba pointi tatu lilifungwa na Moses Phiri dakika ya 65 lilidumu mpaka mwisho wamchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ikumbukwe kwamba Yanga walipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ihefu kwenye ligi msimu wa 2023/24 hivyo watani zao wa jadi Simba wameibuka wababe kwa kukomba pointi tatu.

Kituo kinachofuata ni Novemba 5 Uwanja wa Mkapa, Kariakoo Dabi, Simba v Yanga.