WATATU HAWA HAPA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA YANGA

MAJINA ya nyota watatu wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi yamepenya kuwania tuzo ya mchezaji bora.

Yanga hivi karibuni iliingia ushirikiano na NIC kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo watakaofanya vizuri ndani ya mwezi husika.

Oktoba 28 vinara hao wa ligi wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi saba za ligi wameanza mchakato wao wa kumsaka mchezaji bora wa mwenzi.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga Ali Kamwe amesema kuwa kura zitapigwa na mashabiki kupitia Yanga App.

“Majina matatu ambayo kamati imeyaleta kwa uongozi wa Yanga Kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi, nayo ni Stephane Aziz Ki, Dickson Job pamoja na Max nzengeli, majina haya yatapigiwa kura kupitia Application yetu ya YANGA APP,”.