NDANI ya dakika 180, ukuta wa Azam FC umeruhusu mabao sita katika mechi za Ligi Kuu Bara.
Ilianza dhidi ya Yanga 3-2 Azam FC huku mabao yote Kwa Azam FC yalifungwa na Aziz KI.
Oktoba 28 2023 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-3 Namungo FC.
Mabao ya Namungo FC yalipachikwa na Pius Buswita dakika ya 10, Hasheem Manyanya dakika ya 19 na Reliants Lusajo dakika ya 50.
Bao pekee la Azam FC lilipachikwa kimiani dakika ya 70 na Ayoub Lyanga.