PAN AFICAN KAZINI KWA MARA NYINGINE TENA

KIVUMBI cha Championship kinatarajiwa kuendelea kwa wakongwe kazini Pan African watakapowakaribisha FGA Talents.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 28 kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Nyasi za Uwanja wa Uhuru zitakuwa kwenye kazi saa 10:00 jioni kwa wanaume hao 22 uwanjani kusaka ushindi kwa jasho.

Mchezo wao uliopita ilikuwa ni Oktoba 21 ambapo waligawana pointi mojamoja na Mbeya City Uwanja wa Uhuru.

Kwenye msimamo Pan African ipo nafasi ya 15 ina pointi nne kibindoni huku wapinzani wao wakiwa nafasi ya 12 na pointi nane kibindoni msimu wa 2023/24.