NI Gadiel Michael ndani ya Singida Foutain Gate ana balaa kutoka na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi na kulinda pia.
Sio hivyo tu uzoefu alioupata ndani ya Simba na Yanga unazidi kumpa nguvu ya kuonyesha makeke yake.
Ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Ricardo Ferreira wa Singida Foutain Gate huenda akaanza pia mbele ya mabosi wake wa zamani Yanga, Oktoba 27 2023.
Unakumbuka lile bao lililota utata mchezo dhidi ya Simba dakika ya 58 kwa mwamuzi kutafsiri ilikuwa ni mtego wa kuotea? Krosi majanga ilitoka kwenye mguu wa Gadiel.
Mbali na beki huyo yupo Meddie Kagere ambaye ni mshambuliaji huyu uwezo wake unafahamika akiwa ni miongoni mwa washambuliaji bora wa hivi karibuni kufunga mabao zaidi ya 50 Bongo.
Kagere aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba na sasa yupo zake akipata changamoto mpya Singida Fountain Gate.Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.