DODOMA JIJI KUMEKUCHA, MASHUJAA YAWAKUTA

WAKIWA Uwanja wa Jamhuri, Dodoma walikuwa mashuhuda wakibaki na pointi tatu mazima baada ya dakika 90.

Ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-0 Kagera Sugar iliyokuwa inazisaka pointi tatu pia.

Bao la ushindi ni mali ya Cristian Nzigah aliyepachika bao hilo dakika ya 40 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Ikumbukwe kwamba Kagera Sugar ilitoka kukomba pointi tatu za Mtibwa Sugar kwenye Sugar Dabi baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Manungu ukisoma Mtibwa Sugar 0-2 Kagera Sugar.

Oktoba 25 mechi za ligi zilikuwa kwenye mwendelezo ambapo ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma JKT Tanzania 1-0 Tabora United, Coastal Union 2-0 Mashujaa ilipigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.